URAFIKI WA MAISHA
ni mara nyingi watu hukutana katika shughuli mbali mbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi pamoja na kiutamaduni. mkutano huu mara nyingi kwa hatua ya kwanza hutawaliwa na woga, khofu pamoja na mashaka juu ya mmoja kwa mwengine kwa kua tu ni mara ya kwanza kuonana.
urafiki huzidi kuimarika pale marafiki walioonana kuanza kuoneshana ukarimu pamoja na kuoneshana tunu za nafsi ambazo kimsingi ni adimu na adhim kumuonesha mtu usiemjua.
mahusiano huanza kuzaliwa na kukua mithili ya mti unavyokua, huanza kuchanua maua ambayo hutoa harufu nzuri kwa wale wanaoliangalia.
maua hutoa matunda madogo madogo ambayo kimsingi huwezi kuyatamani ka wakati huo lakini unajenga matumaini ya matumizi ya matunda hayo baadae.
matunda nayo yanapevuka / yanakomaa na kuwa tayari kwa kuliwa. inapofikia hatua hii, kila mmoja kati ya marafiki huwa anajua udhaifu na ubora wa mwenzake.
mwanzo na mwisho wa urafiki huwa unalingana, zile hofu ulizokuwa nazo mara ya kwanza wakati wa kukutana, unakuwa nazo tena wakati munaagana.
unahisi hatotokea mwengine mwenye sifa kama za yule uliemuacha .......
mambo daima hayawi hivyo
tunaonana na tunaachana na tunajenga urafiki na watu wengine kabisa......
na hayo ndio maisha
urafiki wa maisha ndio dhana iliyonisukuma kuandika ujumbe huu..................................................
urafiki wetu uwe wa kuonana na kutengeneza NETWORK- MTANDAO,
kujuana na mtu mmoja tu ni faida kwako....